LIVERPOOL YAKATAA KUWACHUKUA RAFINHA NA GOMES WA BARCA ILI KUMTOA COUTINHO

TIMU ya Liverpool imesema kwamba haina mpango wa kuwasajili viungo wa  Barcelona, Rafinha na Adrew Gomes, kama sehemu ya mkataba wa kumwachia nyota wao,  Philippe Coutinho.

Taarifa hizo zimekuja baada ya tetesi kusambaa nchini Hispania zikieleza kwamba kocha wa Reds, Jurgen Klopp, anajiandaa kuwasajili mastaa hao ambao thamani yao inafikia pauni milioni 36 kwa kila mmoja.


 Hata hivyo, mtandao wa ECHO uliripoti juzi kuwa Liverpool hawana mpango huo kuhusu Mbrazil, Rafinha ambaye anasumbuliwa na majeraha kwa kile wanachodai hana kiwango ambacho  kinafaa kwenye kikosi hicho cha  Klopp.

No comments