LULU DIVA ASEMA WIMBO “MILELE” UMEMPA CHANGAMOTO NYINGI KIMAISHA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Lulu Abbas “Lulu Diva” amesema wimbo wake unaoitwa “Milele” ndio uliompa wakati mgumu tangu alipoanza kujihusisha na tasnia ya uimbaji.

Lulu Diva amesema ugumu ulianza wakati wa kuandaa wimbo huo hadi kukamilisha.

Alisema licha ya kuwa wimbo huo ulimtambulisha vyema katika tasnia ya muziki hapa nchini, lakini ulimpa changamoto kubwa ambazo zimebaki kama kumbukumbu kwenye maisha yake.

“Wimbo wangu wa "Milele" ninauheshimu sana, umenitoa na kutambulisha katika ulimwengu wa muziki, ila ulinipa wakati mgumu sana kuhakikisha unakamilika,” alisema Lulu Diva.


Lulu Diva alisema wimbo huo ambao video yake ilifanyika nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji Nicholaus, ulimpa nafasi ya kufika nje ya nchi kwa mara ya kwanza.

No comments