LWANDAMINA AIBEZA SIMBA SC... asema haina lolote jipya

KOCHA George Lwandamina ambaye anakinoa kikosi cha Yanga kilichobeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo, amesema kwamba kwa muda wote alikuwa akifanya kazi ya kuisoma Simba na kudai kuwa hawana lolote jipya.

Lwandamina amesema kuwa klabu hiyo imekuwa ikizungumzwa zaidi kwenye vyombo vya habari kwasababu ya usajili wake lakini ukweli ni kuwa uwanjani ni wa kawaida sana.

“Simba siyo timu inayoweza kututisha kwasababu nimeifuatilia tangu wakiwa Afrika Kusini, ni timu ya kawaida sana ambayo haiwezi kututisha,” alisema kocha huyo.

“Nadhani wanazungumzwa sana kwenye vyombo vya habari kwasababu ya usajili wa wachezaji ambao imewanasa lakini haina maana kuwa ni klabu inayotisha,” aliongeza kocha huyo.


Simba na Yanga zinatarajia kukutana katika mechi ya kuwania ngao ya hisani Agosti 23, mwaka huu kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara.

No comments