LWANDAMINA AJIPA UHAKIKA WA KUIMALIZA SIMBA KWA ASILIMIA ZOTE KESHO

KOCHA mkuu wa kikosi cha Yanga George Lwandamina raia wa Zambia amesema haoni sababu ya msingi itakayomzuia asiweze kubeba Ngao ya Hisani katika mechi ya kesho dhidi ya mahasimu wao Simba.

Lwandamina alidai kuwa kwa kiasi kikubwa kikosi chake kipo fiti baada ya kuweka kambi kwa muda mrefu Zanzibar hivyo suala la ushindi ndio kipaumbele chake.

“Nafahamu mechi hizi zimejaa presha kubwa lakini nina uzoefu nazo na kwangu mimi nachukulia kama zilivyo mechi nyingine ila ikikubwa nahitaji kubeba kombe hili ili kutoa ishara ya kuanza vema michuano ya Ligi” alisema kocha huyo.


“Hali ya kikosi ipo shwari na hata kambi yetu ina mazingira tulivu kiasi hivyo nina kila sababu ya kuhakikisha tunashinda ukizingatiakuwa tumekaa pamoja kwa muda mrefu hata kabla ya kuja hapa” aliongeza.

No comments