MAANDALIZI YA SHOW YA CHRISTIAN BELLA BL PARK SI YA KITOTO …Jukwaa lafungwa siku mbili kabla


Hakuna ubishi kuwa hili ni tukio litakaloacha historia kubwa kutokana na maandalizi ya ‘kisomi’ yanavyoendelea kufanyika.

Show ni Jumamosi hii Agost 19, pande za Tabata Kinyerezi ambapo litafanyika onyesho kubwa la mfalme wa masauti Christian Bella akiwa na bendi yake ya Malaika ndani ya kiota cha maraha cha BL Park.

Kuanzia Alhamisi usiku, jukwaa kubwa na la kisasa la onyesho hilo, lilianza kufungwa, hali inayoashiria kuwa waandaaji wamepania kuandika historia.

Onyesho hilo ni maalum kwaajili ya utambulisho wa nyimbo tatu mpya za Bella “Shuga Shuga”, “Niende Wapi” na “Punguza Kidogo” ambazo bado hazijaachiwa hewani.

Mratibu wa onyesho hilo Issa Mwendapole aliiambia Saluti5 kuwa watabadilisha kabisa madhari ya BL Park kwa kuzungusha uzio mkubwa, jukwaa la kisasa, mapambo bab kubwa, unadhifu pamoja na ‘sound’ si ya kitoto.

Tayari ukweli wa kauli ya Issa Mwendapole umeanza kuonekana kufuatia ushahidi huu wa picha za ufungwaji wa jukwaa kubwa na la kisasa.
No comments