Habari

MAKALA YA CHIKI MCHOMA: RAIS WALLACE KARIA FANYA UFANYAVYO LAKINI TURUDISHIE MPIRA WETU

on

Wimbo mbaya
haubembelezewi Mwana.. Wahenga tulishatoa tamko siku nyingi..!!
Wimbo huu wa
Turudishie mpira wetu ndio wimbo uliokubalika na ukaimbwa na ukaimbika Vyema
kabla  na Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa
Nafasi ya Urais na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira nchini
yaani TFF.
Baada ya
Uchaguzi kwisha na Wimbo huu umezimwa au kuzimika ghafla.
Lakini kwa
wenye Akili wimbo huu bado unaimbwa na unaimbika Vyema kabisa vichwani Mwao.
Hakuna ubishi
kuwa wimbo huu uligeuka kuwa Wimbo wa Wananchi wa Tanzania kwa jinsi kelele
zilivyokuwa zikisikika haswa Mitandaoni na kwenye Vyombo vingi vya Habari.
Huu ndio
wimbo uliokuwa bora zaidi kuelekea Uchaguzi ule.
Hata Rais
Karia anajua hilo…!!!
Ubaya wa
Wimbo Ule.
Wimbo ule
ulijaa maneno mengi yasiyo na tafsiri ya moja kwa moja hivyo kuhitaji watu
wenye vichwa vipana sana kukubaliana na Tafsiri iliyokusudiwa.
Wimbo ulijaa
maneno mengi yasiyofafanulika kirahisi kiasi kila mtu akautafsiri ajuavyo
lakini wimbo ule ulibakia kuwa Wimbo bora na Ulioogofya kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa TFF.
Wengine
waliutilia Mashaka kuwa wimbo ule ungewaathiri katika utekelezaji wake kwa kuwa
baada ya muda fulani wenye kuudai mpira wao wangepoka nafasi zao na kuzimiliki.
Hii iliogofya
na kusababisha Falsafa ya ‘Tujilinde Kwanza’ itumike.
Na ilitumika
Vyema.
Uzuri Wa
Wimbo Ule :
Wimbo ule
unaishi…!!!
Wimbo ule
hauchuji na wala hauoneshi ipo siku utachosha watu kuuimba…!!
Wimbo ule
umejaa Falsafa kamili ya Uhitaji wa watu…!!
Haukwepeki
Kuuimba.. Utake.. Usitake… Utauimba hata Kimoyo Moyo…!!!
Ngoja
nifungue Mabano…!!
Rais Karia
amekuwepo kwenye Maisha ya Mpira wa Tanzania kwa miaka mingi mno kuliko wengi
walivyodhani.
Hakuwa mtu wa
kujikweza wala mtu wa Vyombo vya Habari wala Mtu aliyetafuta sifa binafsi…
Hapana..!!!
Na ndio maana
hata waliokuwa wakimpinga nje ya Ulingo walimpinga kwa hoja dhaifu kuwa yeye ni
Miongoni mwa walalamikiwa kwa ”Upotevu wa Mpira wao”… Hoja Dhaifu..!!!
Wajuzi na
Wanaomjua Rais Karia wanasema ‘Alitengwa na Mfumo’.. Lakini alikuwa ni mtu bora
zaidi kiutendaji na aliamini katika mpangilio na sio ‘twende tufanye’.
Hii ilimfanya
akae mbali na Mfumo kisha aandae kile anachokiamini kuwa ni bora zaidi kuelekea
Mafanikio makubwa aliyoyatamani.
Na ndio maana
hakuogopa kuchukua fomu mbele ya ‘Rais’ wake aliyekuwa nae.
Wenye
kufikiri… Watajiongeza hapa…!!!
Hata kilele
cha Uchaguzi kilipofika tayari Wajumbe 95 kati ya Wajumbe 131 waliostahili
kupiga kura walishakuwa na Maamuzi.
( Bado
namtafuta Kocha Muhibu Kanu ili anipe Siri ya kupatikana kwa kura hizi.)
Nilipomuona
Ally Mayai Tembele na Shafih Dauda wakihojiwa.. Kwa bashasha waliyokuwa nayo…
Nilihisi kabisa bado tuko salama..!!!
Hawakuonesha
mashaka wala hofu yoyote juu ya Mchakato… Waliridhia…!!!
Ally aliibeba
kauli mbiu iliyogusa hisia za Mashabiki wa Soka na ni Kauli mbiu hiyo ambayo
Rais Karia anawajibika kuitekeleza kwa kuwa ndiyo hisia kamili za Mashabiki.
Si
dhambi…!!
Tumeshuhudia
hata kwenye Siasa za Nchi yetu ‘Mabadiliko’ yalipohitajika hayakuchagua nani
kaanzisha neno hilo bali Tafsiri halisi ya kinachoitwa ‘Mabadiliko’ ndicho
kinachoendelea kufanyiwa kazi…
Si dhambi kwa
Rais Karia kuijua Vyema Falsafa ya Kurudisha Mpira na Kuifanyia kazi kikamilifu
hata kwa kukaa chini na Muasisi wa Kauli mbiu hiyo na kumtaka washirikiane
kuitafsiri kivitendo zaidi..
Si
Dhambi…!!
Rais Karia
yupo kwa ajili ya Watanzania wote na hadi hapo alipo ajue tu kuwa anatekeleza
dhana iliyojificha kuwa ipo sehemu tunakosea au tulikosea… Atusaidie
kuifichua…!!
Rais Karia
kwa kuwa amedhihirisha si mtu wa Makundi na wala hana ‘Watu Wake’… Tunamuomba
Aturudishie Mpira Wetu…!!!
Rais Karia
ajue hana dosari na wala asiitafute dosari abaki kuwa Baba wa Mpira na Wapenda
mpira wote.
Turudishie
mpira wetu Mashuleni na Vyuoni uchezwe kwa Ufundi na Weledi kwa kuwa Makocha
wenye Vigezo ni Wengi.
Turudishie
mpira wetu kwa kulazimisha uwepo wa Wakurugenzi wa Ufundi kwenye kila timu ya
Ligi Kuu na Hata Daraja la Kwanza.
Turudishie
Mpira wetu kwa kuweka Kitengo maalum cha wataalam wa Masoko ili kushawishi
Makampuni makubwa ya Ndani na Nje ya Nchi kuwekeza kwenye Soka nchini katika
ngazi zote.
Turudishie
mpira wetu kwa kuwa na ligi zinazochezwa nchi nzima kuanzia ngazi ya Kata.
Turudishie
mpira wetu kwa kuwa na Soka la Mkoa kwa Mkoa ili kurudisha uwezo wa Mikoa kuwa
na timu ngumu na zenye uwezo wa kushindana na timu za Kariakoo.
Nina mengi ya
kutaka uturudishie kwenye Soka ila najua nawe una mengi uliyopanga yarudi kwenye
Soka!!!.
Slogan
Covered…!!!
Nawasilisha.
Imeandikwa na Chiki
Mchoma

+255 712 885
999.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *