MAMIA WAMZIKA DJ IDEED MAKABURI YA KINONDONI


DJ Ideed Yussuf,  mmoja kati ya waanzilishi wa harakati za muziki wa kizazi kipya Tanzania, ambaye alifariki ghafla jana asubuhi, amezikwa leo saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Marehemu alianza kulisongesha gurudumu la muziki wa kizazi kipya kupitia kundi la  Mobb & Genius FBI la Kinondoni katikati ya miaka ya 90.

Baadae marehemu akaibukia kwenye u-DJ katika maeneo kadha wa kadha jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa ofisi zake za karibuni ni  Twitter Bar, Meridian Hotel na Papi Chulo zote za Kinondoni.

Taarifa za awali zilizofikia Saluti5 zilidai kuwa hadi  Jumapili usiku marehemu alikuwa mwenye afya njema akishiriki kupiga muziki katika pub mpya iliyofunguliwa jirani na Twitter Pub, kabla ya kuzidiwa ghafla na kukimbizwa Mwananyamala Hospital alipotibiwa hadi mauti yalipomkuta Jumatatu asubuhi.

Mazishi ya DJ Ideed yalihudhuriwa na umati mkubwa miongoni mwao akiwemo diwani wa kata ya Mwananyamala Mh. Songoro Mnyonge na mbunge wa mikumi Mh. Joseph Haule  "Profesa Jay"  pamoja na wasanii wengi bila kumsahau paparazi maarufu wa Kinondoni, Jobu Faustine "Mwewe".
Sehemu ya umati uliofika kwenye mazishi ya Ideed
 Katikati ni Dj Elly 4x4 wa Clouds FM
 Professa Jay akiwa na Fid Q kwenye mazishi ya Dj Ideed
 Sehemu nyingine ya umati uliohudhiria mazishi ya Dj Ideed
 Mbunge wa Mikumi Proffesa Jay (katikati) akiwa mazishini
 Wasaa wa dua
Msanii wa filamu na muziki Hemed PHD (kushoto) naye alikuwepo

No comments