MANCHESTER CITY KUMSAJILI JONNY EVANS BEKI WA ZAMANI WA MAN UNITED


Manchester City imepeleka ofa ya pauni milioni 18 kwaajili kumnyakua sentahafu Jonny Evans lakini klabu yake ya West Bromwich Albion imeipiga chini ofa hiyo na sasa kocha wa City Pep Guardiola anajiandaa kuongeza dau.

Guardiola anataka kuongeza beki wa kati baada ya kuamua kutumia mfumo wa kuchezesha masentahafu watatu.

Huku Eliaquim Mangala akiwa mbioni kupigwa chini, City inabakiwa na John Stones, Nicolas Otamendi na Vincent Kompany ambao wote walicheza katika mchezo wa kwanza wa Premier League dhidi ya Brighton Jumamosi iliyopita.

Guardiola anamuona Evans, beki wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 29, kama chaguo sahihi la mfumo wake wa kuchezesha mabeki watatu wa kati.
No comments