MANCHESTER UNITED MBIONI KUTIA HISA ZAKE SOKONI NEW YORK

WAMILIKI wa timu ya Manchester United, Familia ya Glazer wanatajwa kuwa mbioni kuuza hisa za timu hiyo katika soko la Hisa lililopo New York.

Mabosi hao wamependekeza kuuzwa asilimia mbili tu ya sehemu ambayo wanaimiliki kwa kiasi cha Pauni Milioni 56.04. Hadi kufika siku ya Jumanne zoezi hilo linatarajiwa kumalizika.

Mchakato huo utahusisha uwiano wa hisa ambazo zitapigiwa kula na wahusika kwenye Soko la Biashara la Marekani. Kura zikivuka asilimia 20 itakuwa rasmi imeuzwa kwa muhusika atakayeinunua.


Familia ya Glazer waliinunua Manchester United mwaka 2005 kwa Pauni Milioni 790. Mwaka 2010 waliuza asilimia 10 ya hisa zao. Huku wakiwa mbioni kuuza zingine tena kwa siku zijazo.

No comments