MAPACHA MUSIC BAND NDANI YA MASAI CLUB WEE WACHA TU …Chaz Baba, Jose Mara pacha hatari


Moja ya viwanja safi kwa burudani siku za Jumapili Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni, ni mojawapo ambapo utakula ladha adimu kutoka kwa Mapacha Music Band chini ya Jose Mara.

Jumapili usiku Mapacha Music Band wakatandika show moja yenye akili sana ndani ya kiwanja chao hicho cha kila Jumapili, huku mahudhurio ya mashabiki yakiwa mazuri kiasi kwamba ukumbi ule ulionekana ni mdogo kulidhibiti onyesho lile.

Alikuwepo msanii mwalikwa Chaz Baba ambaye aliposimama na Jose Mara, swahiba wake wa tangu utotoni, ikawa ni burudani juu ya burudani.

Wawili hao wakaonyesha kwamba wanaposimama pamoja unapata pacha moja ya hatari sana katika ulimwengu huu wa muziki wa dansi, jamaa walifunika sana.

Wakati Mapacha wakiimba wimbo wao “Dunia Simama” ukingoni kabisa mwa onyesho lao, mashabiki nao ni kama vile walikuwa wanaomba muda usimame ili waendelee kupata uhondo wa Mapacha Music Band.
 Chaz Baba akikamua kwenye jukwaa la Mapacha Music Band
 Jimmy Gola mwimbaji anayekuja juu kwa kasi
 Jose Mara na Chaz Baba wakimimina uhondo
 Jose Mara 
 Kulia ni Sam wa Mapacha akiimba sambamba na Chaz Baba
Ilikuwa ni hatari lakini salamaNo comments