MAPACHA MUSIC BAND WAKO TEGETA IDD MOSI …Jose Mara na Chaz Baba wana lao jambo, Idd Pili ni Sinza


Mapacha Music Band, moja ya bendi bora kabisa za dansi hapa nchini, Idd Mosi itakuwa Tegeta ikizindua ukumbi mpya.

Bosi wa Mapacha, Jose Mara ameiambia Saluti5 kuwa ukumbi huo unaitwa The One Hall ambao uko jirani kabisa na kituo cha Tegeta.

Burudani ya Mapacha itanogeshwa na msanii mwalikwa Chaz Baba swahiba mkubwa wa Jose Mara.

Siku ya Idd Pili, Jumamosi hii Mapacha watashusha mzigo wa burudani ndani ya kiota kingine kipya Green Lounge, Sinza jirani na Igo Lounge.

Jose Mara amesema hata onyesho la Idd Pili nalo pia ni la uzinduzi wa ukumbi mpya ambapo huko nako pia atakuwepo Chaz Baba.

“Kumbi zote hizi mbili (The One Hall na Green Lounge) zinamilikiwa na mtu mmoja”, alisema Jose Mara na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kila mtu kupambana na hali yake.

No comments