MAPACHA WATATU YA CHOKORAA KUIBUKIA KWA MAMA MWENYE NYUMBA MANGO GARDEN IDD MOSI


Bendi iliyozaliwa upya - Mapacha Watatu chini ya Khalid Chokoraa, siku ya Idd Mosi itatumbuiza ndani ya Mango Garden Kinondoni, ukumbi wa nyumbani wa Twanga Pepeta ya mamaa Asha Baraka.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Chokoraa kuvamia ngome ya Twanga Pepeta tangu alipoitema kimtindo bendi hiyo takriban mwezi mmoja uliopita.

Akiongea na Saluti5, Chokoraa amesema siku hiyo watatambulisha nyimbo mpya kabisa ambazo zitaingia radioni hivi karibuni.

“Hii ni fursa kwa wana wa Kinondoni kuja kushuhudia bendi mpya, nyimbo mpya pamoja na zile za zamani zilizotamba chini ya utunzi wangu ndani ya makundi mbali mbali niliyoyatumikia”, alisema Chokoraa.

No comments