"MARCEL SCHMELZER AMEANZA KUJIFUA KWA AJILI YA MSIMU UJAO" DORTMUND WATHIBITISHA

VINARA wa soka katika michuano ya Ligi Kuu Ujerumani,  Bundesliga,  Borussia Dortmund  wamethibitisha kuwa nyota wao, Marcel Schmelzer ameanza kujifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Vinara hao walitoa  taarifa hiyo juzi, lakini wakasema kuwa licha ya  Schmelzer kuwa ameanza mazoezi mepesi lakini hajapona kabisa.

Baada ya msimu uliopita nyota huyo kucheza mechi 26 nahodha huyo alipata majeraha ya enka wakati akiwa katika michuano ya Mabingwa wa Kimataifa barani  Asia.

Taarifa za kuumia kwake zilieleza kuwa staa huyo mwenye umri wa miaka  29 angekaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne jambo ambalo linamfanya aanze kujinoa vikali ili aweze kuwa fiti kwa ajili ya mechi ya kwanza ya  Dortmund dhidi ya  Wolfsburg ambayoitapigwa Agosti 19 mwaka huu.


Kwa sasa mastaa Marco Reus, Julian Weigl na  Raphael Guerreiro  tayari wameshaonekana kuwa watazikosa mechi za mwanzoni mwa msimu ujao, lakini ujio wa Schmelzer inaweza kuwa habari njema kwa kocha wao mpya Peter Bosz.

No comments