MARCO VERRATTI AKIRI KUTETA NA BARCELONA

NYOTA wa timu ya Paris Saint-Germains, Marco Verratti amekiri kuteta na Barcelona ‘lakini akachomoa  huku akikanusha kuwa ujio wa staa waoa mpya  Neymar ndicho kilimfanya abaki.

Barca nao walishaweka wazi kumsaka kiungo huyo wa timu ya Taifa ya  Italia ambaye naye alikuwa tayari kuondoka ili akasake mahali ambapo anaweza kutwaa ubingwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo uhamisho huo haukufanikiwa  baada ya PSG r kuvunja mkataba wa  Neymar kwa gaharama ya Euro milioni 222 na huku Verratti mwemye mkataba na klabu hiyo hadi mwaka   2021 akikisisitiza anajisikia mwenye furaha kuendelea kuishi katika mji mkuu huo wa Ufaransa.


"Barcelona?  Yalikuwapo majadiliano, lakini hakufika mbali ," Verratti said alikaririwa na Sky Sport Italia akisema. "Hatukuweza kufikika muafaka wowote na ndio maana nikaamua kubaki  na kama kuhusu  Neymar  ndiye aliynibadili mawazo yangu sio kweli kwani nilifanya hivyo kabla hajasajiliwa,”alisema staa huyo.

No comments