MASHABIKI WA YANGA WAMMIMINIA SIFA KABAMBA TSHISHIMBI

KIUNGO Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasa ya Kongo (DRC), alikuwa gumzo kwenye jukwaa la mashabiki wa Yanga baada ya kuonyesha uokovu katika mechi yake kubwa ya kwanza iliyochezwa katika dimba la uwanja wa Taifa.

Tshishimbi alikuwa nguzo muhimu katika kusaidia kupunguza presha ya mashambulizi ya Simba ikiwa ni pamoja na kuokoa hatari kadhaa ambazo zingezaa mabao katika mchezo huo wa kuwania Ngao ya Jamii.

Mashabiki wa Yanga walisikika wakisifu kiwango chake wakati wote wa mchezo ambapo ali0nekana akifanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi ya Simba.

“Hawa ndio watu tuliokuwa tukiwahitaji miaka mingi hata hela iliyotolewa kumsajili haiumi, ni mchezaji anayejielewa na mkakamavu katika mechi ngumu,” alisikika shabiki aliyejulikana kwa jina moja la Juma.

“Ni kweli tumepoteza mchezo kwa njia ya penalti lakini kwa kelele zilizokuwa zikipigwa na Simba kabla ya mchezo ungedhani wakija uwanjani watafanya kitu kikubwa kumbe ni wa kawaida tu, Tshishimbi peke yake anawatosha,” aliongeza shabiki huyo.


Simba na Yanga zilikutana juzi katika mchezo wa kuwania Ngao ya Hisani ambapo wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa njia ya matuta.

No comments