MASHAUZI CLASSIC KUUNGURUMA OPEN AIR KAWE IDD MOSI … “Thamani ya Mama” ndiyo habari ya mjini


Kundi la Mashauzi Classic chini ya Jike la Simba Isha Mashauzi, limeweka hadharani ratiba yao ya sikukuu ya Eid el Hajj ambapo Idd Mosi wataunguruma Kawe, jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Saluti5, Isha Mashauzi amesema onyesho hilo maalum la Eid El Hajj litafanyika Ijumaa hii ndani ya ukumbi wa Open Air.

Isha amesema mkesha wa Idd, Alhamisi watakuwa kwenye ukumbi wao wa nyumbani – Mango Garden Kinondoni.

Moja ya zawadi watakayoipata wakazi wa Kawe na maeneo ya jirani, ni wimbo mpya kundi hilo, “Thamani ya Mama” ulioimbwa na Isha Mashauzi.


Wimbo huo ulioachiwa hewani wiki tatu zilizopita, kwasasa ndiyo habari ya mjini kwa upande wa nyimbo za taarab kwa namna ulivyopekwa vizuri radioni hadi mitaani.

No comments