MASHAUZI CLASSIC WAJA NA "USIKU WA THAMANI YA MAMA" MANGO GARDEN

SHOO kubwa inayokwenda kwa jina la ‘Usiku wa Thamani ya Mama’ inatazamiwa kukung’utwa na Mashauzi Classic Modern Taarab leo Alhamisi ndani ya Mango Garden Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Sumalagar ameinyetishia Saluti5 kuwa shoo hiyo inatazamiwa kuwa ya kukata na shoka kutokana na maandalizi makubwa yaliyofanywa.

“Nawaomba mashabiki kuja kwa wingi katika shoo hii ambayo kiingilio chake kitakuwa ni sh. 5,000 tu na ambayo itaanza kurindima majira ya saa 3:30 usiku na kuendelea hadi majogoo,” amesema Sumalagar.


“Kutakuwa pia na surprise kibao kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki Bongo, hivyo si ya kukosa hata kidogo kwani shabiki atakayekosa atakuwa amekosa kitu muhimu zaidi.”

No comments