STAA mpya wa Manchester United, Nemanja Matic  juzi aliamua kuitumia siku yake ya kuzaliwa kwa kuzunguka katika jiji  la Manchester akiwa na mkewe, Aleksandra ili kutafuta makazi mapya.

Staa huyo alimiza umri wa miaka 29 juzi wakati akitafuta pia nyumba mpya katika eneo la Cheshire  ambako anataka aishi na familia yake baada ya kuingia mkataba na mashetani hao wekundu.


Kwa mujibu wa gazeti la Dail Mail, mchezaji mwenzake,  David de Gea  ndiye aliyekuwa wa kwanza kumkaribisha baada ya kutuma ujumbe kupitia katika mtandao wake wa kijamii akimtakia kila la kheri katika  siku ya kuzaliwa kwake.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac