Habari

MAYWEATHER ATAJA KITAKACHOMPA WAKATI MGUMU PAMBANO LAKE NA MCGREGOR AGOSTI 26

on

BINGWA wa ngumi uzito wa juu, Floyd Mayweather, amesisitiza kuwa
umri wake unaweza kumpa wakati mgumu katika pambao lake dhidi ya Conor
McGregor, Agosti 26 mwaka huu.
Mayweather amesema, anaamini
pambao hilo litakuwa na ushindani wa aina yake lakini litakuwa tofauti na lile
la miaka miwili iliopita dhidi ya Manny Pacquiao.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika
kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena, mjini Las Vegas, Marekani, lakini Mayweather
amedai mpinzani wake McGregor ana nafasi kubwa ya kuwa mshindi.
“Mpinzani wangu ana umri mdogo
sana, ana miaka 29 na mimi nina miaka 40, ukiangalia kuna tofauti kubwa kati
yetu, hivyo ninaelekea kuchoka na yeye bado ana nafasi ya kuendelea kuwa kwenye
ushindani kwa kipindi kirefu.

“Naweza kusema kwamba mimi ni
mzee sasa, nipo tofauti sana na miaka miwili iliopita, hivyo chochote kinaweza
kutokea kwenye pambano hilo, kila mmoja ana lengo la kushinda ili kuweka
historia yake,” alisema Mayweather

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *