MAYWEATHER ATUMIA DOLA MIL 2 KUSHEREHEKEA USHINDI WAKE DHIDI YA CONOR MCGREGOR

BONDIA wa uzito wa kati, Floyd Mayweather, usiku wa juzi ametumia dola za Marekani milioni 2  kusherehekea ushindi dhidi ya mpinzani wake, Conor McGregor.

Kabla ya sherehe hiyo, iliyofanyika muda mfupi baada ya pambano hilo, Mayweather aliwataarifu  mashabiki wake  milioni 17.6 katika ukurasa wake wa Instagram kwamba alikuwa Club ya usiku ya Vegas Strip ‘Girl Collection’ akila bata na marafiki.

Akiwa katika klabu hiyo, muda mwingi Mayweather alionekana akipiga picha na mashabiki wake waliokuwa wakimpongeza kwa ushindi wake huo.

Pambano dhidi ya McGregor lilikuwa likijulikana kama ‘Money Fight’, ambapo Mayweather aliweka kibindoni kiasi cha dola za Marekani milioni 350.

Mpinzani wake alichukua dola milioni 30 kutoka katika pambano hilo na fedha nyingine za ziada ambapo zikijumlishwa  atachukua dola milioni 75.
  
Bondia huyo, ambaye alipigwa KO mzunguko wa 10 katika ulingo wa Mobile Arena, alijumuika na marafiki zake katika klabu nyingine ya Encore Beach Club saa 9:00 usiku na kutoa kiasi cha pauni 77,643 kulipia bili ya vinywaji.


Mayweather, aliyeweka rekodi ya kushinda mapambano 50 bila kupigwa, alijumuika na mashabiki wake akitumia gari lake la kifahari aina ya Bugatti Grand Sport Convertible la mwaka 2012, lenye gharama ya dola milioni 3.

No comments