MAYWEATHER: NIMECHEZA KAMARI KUKUBALI KUREJEA TENA ULINGONI

BONDIA Floyd Mayweather amekiri kuwa, amecheza kamari kubwa kukubali kurudi tena ulingoni kupambana na Conor McGregor, lakini ana uhakika hatapoteza pambano hilo.

Mayweather anashikilia rekodi ya kutopoteza pambano katika kipindi cha miaka 21, alistaafu ngumi Novemba 2015, baada ya kumchapa kwa pointi mpinzani wake, Andre Berto.

Lakini kwa mshtuko mkubwa, Mei 2017, Floyd alitangaza kurejea tena ulingoni kupambana na McGregory, bingwa wa mchezo wa MMA.

“Ni kweli kabisa naamini nimecheza kamari kubwa maishani mwangu,” alisema Mayweather, kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari. “Lakini kuna zawadi kubwa sana kwetu.


“Nimepigana mara 49 na sijapoteza, lakini najua nikipigwa watu watasema sikuwa lolote. Hilo sijali kwa sasa, nataka kupigana kwa ajili ya kuendelea kulinda heshima yangu na mchezo wa masumbwi kwa ujumla,” aliongeza Maywether, kuelekea pambano hilo litakalofanyika Agosti 26, katika ukumbi wa TA, Las Vegas.

No comments