MBARAKA YUSUPH ATAMANI KIATU CHA SIMON MSUVA

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Mbaraka Yusuf amesema ndoto zake ni kumfikia Simon Msuva ambaye alikuwa mmoja kati ya wafugaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu uliopita.

Mbaraka amesema kuwa tangu ajiunge na Azam amekuwa na furaha kutokana na kupata mahitaji yote ya msingi hivyo anaamini kila alichopanga kitafanikiwa.

“Nimejipanga kufanya vizuri zaidi kuliko msimu uliopita naomba Mwenyezi Mungu akinijalia kila mechi nitakazyocheza niweze kupata nafasi, niweze kufunga na kuwa mfungaji bora wa Ligi kama alivyofanya Msuva,” amesema.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Azam FC akitokea Kagera Sugar amesema anajua msimu ujao utakuwa na changamoto kubwa kwake lakini hilo sio kikwazo kwake.

Azam ni timu yangu ya tatu kuichezea kwenye Ligi kwa hiyo nina uzoefu na wakutosha,” aliongeza.


Mbaraka amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo msimu uliopita alifunga mabao 12 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi.

No comments