MFUMO MPYA WA UPIGAJI PENATI WAMSONONESHA GARY CAHILL

NAHODHA wa Chelsea, Gary Cahill ameonyesha kutofurahishwa na mfumo mpya wa upigaji penalty ambao utaanza kutumika msimu huu kwenye Ligi Kuu England.

Chelsea walitumia mfumo huo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Arsenal, lakini walikosa mikwaju miwili ya penalty baada ya nahodha huyo kufunga ya kwanza kwa ustadi mzuri.


“Kabla tulijaribu kufanya mazoezi ili kuuzoea lakini wengi wetu hawakufurahishwa na mfumo huu. Kila mtu alionekana kushangaa jinsi mfumo ulivyo. Niseme ukweli tu, huu mfumo hauvutii kabisa. Utazoeleka kama tutautumia mara kwa mara ila ule mfumo wa kwanza ulikuwa bomba zaidi” alisema Cahill.

No comments