MKE WA WAYNE ROONEY ATAMBA KUWA NA UJAUZITO MWINGINE

MKE wa nyota wa timu ya Everton, Wayne Rooney, Coleen Mary amesema kuwa kwa sasa ana ujauzito mwingine.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ametangaza habari hizo kwa wafuasi wake milioni 1.25  kupitia kwenye matandao wake wa kijamii  Twitter na kusema kwamba anaweza kuwatangazia watu kwani amepimwa na kuchunguzwa vyema.

"Nina furaha sana!!! ..... Sijawahi kukanusha habari hizi, lakini nilikuwa ninazilinda vyema. Nimepimwa  na kuchunguzwa na kila kitu kiko sawa...Mtoto wa nne  yupo njiani."aliandika katika ukurasa wake huo wa Twitter na huku zikiungwa mkono na Rooney  ambaye aliyehamia klabu ya Everton msimu huu.

Coleen na Wayne walifunga ndoa mwaka 2008 baada yao kuchumbiana wakiwa bado vijana wadogo Liverpool.


Wana watoto watatu wa kiume - Kai, wa miaka minane, Klay, wa miaka minne, na Kit, aliyezaliwa Januari 2016.

No comments