MOSI SULEIMAN ASEMA ZANZIBAR STARS NDIO MPANGO MZIMA

MWIMBAJI mahiri wa Zanzibar Stars Modern Taarab, Mosi Suleiman amesema kuwa bendi yake hiyo anaipenda zaidi ya zote alizowahi kuzitumikia tangu aanze kujitumbukiza kwenye muziki.

Mosi aliyasema hayo wiki hii jijini Dar es Salaam katika mazungumzo maalum na Saluti5, ambapo alieleza kuwa ana sababu nyingi za kuipenda Zanzibar Stars lakini kubwa ni namna ilivyomtoa mbali.

“Unajua kabla ya Zanzibar Stars hakuna mtu aliyekuwa anamfahamu Mosi,” alisema staa huyo na kuongeza. “Lakini kwa kupitia nyimbo mbalimbali nilizorekodi hapa nimetokea kuwa maarufu na kupendwa zaidi na mashabiki.

“Nashukuru sasa ninaheshimika mno na nimekuwa nikijiongezea mashabiki kila uchao huku sababu kubwa ikiwa ni Zanzibar Stars, hivyo acha niseme wazi kuwa hii ndio bendi ninayoipenda sana hapa nchini.”


Zanzibar Stars imeibuka upya hivi karibuni ikiwa na kasi ya ajabu ambapo imekuwa ikifanya shoo ya mafanikio ndani ya DDC Kariakoo kila wiki katika siku za Jumanne na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki.

No comments