MOURINHO AMVNJIA UKIMYA ANTONIO CONTE… asema hana muda wa kumzungumzia

KOCHA  Jose Mourinho amemjibu  mwenzake wa Chelsea,  Antonio Conte kuhusu kauli yake aliyoitoa juzi kwamba anaangaika ili kukwepa yaliyomkuta mtangulizi wake huyo wakati akiwa  Stamford Bridge, baada ya kusema hawezi kupoteza pumzi yake  kuzungumza kuhusu Muitaliano huyo.

Kwa sasa  Chelsea kujaribu  kunyakua tena yaji lake ililolichukua msimu uliopita na tayari  Conte ameshawaonya wachezaji wake kukaza buti ili wasije wakakumbwa na msimu kama wa Mourinho  ambao  Blues walishika nafasi ya 10 wakuwa chini ya kocha wa muda  Guus Hiddink na huku Mreno huyo akiwa ameshafukuzwa kabla ya sikukuu ya Krismas baada ya kuonesha kiwango kibovu.

Akizungumza juzi mara baada ya kuondoka na ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya  Valerenga katika mechi ya kirafiki,Mreno huyo alisema kuwa anachoweza kukizungumza kwa sasa ni kuhusu timu yake  kutokana na kwamba anafahamu vyema jinsi alivyokuwa akipambana na Juventus na wachezaji raia wa Italia.

 "Sifahamu.Lakini naweza kujibu kwa njia tofauti, lakini siwezi kupoteza pumzi yangu kuzungumza kuhusu  Antonio Conte,"alisema Conte.

Juzi Man United  walendelea kuonesha kiwango kizuri katika michezo yake ya kujiandaa na msimu ujao tangu walipofungwa na  Barcelona  kwa kushinda mchezo huo wakishukuru mabao yaliyowekwa kimiani na mastaa wao, Marouane Fellaini, Romelu Lukaku  na Scott McTominay.


Huku wakiwa bado wanamchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya  Sampdoria  utakaopigwa kesho kabla  yaw a  UEFA Super Cup  dhidi ya  Real Madrid, Mourinho  alisema kuwa anakunwa mno na maanadalizi ya timu yake hiyo.

No comments