MOURINHO AMWEKA GARETH BALE KIPORO

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, anaripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili straika wa Real Madrid, Gareth Bale, lakini si mwaka huu bali ni mwakani.

Mreno huyo anasemekana anamtaka raia huyo wa Wales, lakini anafahamu hana nafasi ya kufanya hivyo katika dirisha la usajili la sasa na kwa mujibu wa gazeti la  Express atajaribu kumpeleka Old Trafford mwaka ujao.

No comments