MRITHI WA SHAABAN DEDE MSONDO KUANIKWA USIKU WA DIMBA CONCERT


BENDI kongwe ya Msondo Ngoma, inatarajia kumtambulisha rasmi mwimbaji atakeyechukuwa nafasi ya aliyekuwa mwanamuziki wa bendi hiyo Shaaban Dede aliyefariki Julai 6, mwaka huu.

Tukio hilo la kihistoria linatarajiwa kufanyika Septemba 2 mwaka huu katika ukumbi wa Travertine Magomeni ambapo bendi hiyo itaumana na wanamuziki maarufu Tanzania wanaounda kundi linalojulikana kama Timu ya Taifa ya muziki wa dansi Tanzania.

Msemaji wa bendi hiyo Juma Katundu amesema kwamba utambulisho wa mwanamuziki huyo utakwenda sambamba na mashabiki kumshuhudia akiimba moja ya nyimbo alizokuwa akiimba Dede.

Hata hivyo Katundu hakutaka kuweka wazi jina lake kwa madai kwamba wamepanga liwe ni tukio la kushangaza mashabiki ambalo litafanyika siku hiyo tu.

Katika hatua nyingine Katundu alisema, kikosi chao chini yawanamuziki wakongwe waliochanganyika na vijana watahakikisha wanalisambaratisha kundi hilo la wanamuziki hatari licha ya kwamba wanawaheshimu.

No comments