MSAMI AAMUA KUANIKA KAZI YAKE INAYOMVUTIA ZAIDI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Msami Giovan amesema katika kazi zake zote alizowahi kufanya hadi sasa, wimbo unaomvutia na kumpa hisia kubwa ni “Step by Spep.”

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msami amesema wimbo huo umekuwa ukumvutia kila anapousikia hasa katika upande wa sauti za vinanda.

Alisema kazi hiyo imekuwa ikimburudisha na kumpa faraja ya kuendelea kujituma zaidi ili kuhakikisha anafika mbali katika tasnia ya muziki.

“Step by Step ni wimbo wangu ambao umekuwa ukinipa faraja sana, si kwamba kazi zangu nyingine nilizofanya hazivutii hapana, ila vinanda na zile sauti za vifaa mbalimbali vilivyotumika ndani ya wimbo huo ni sababu,” alisema Msami.

Msami alisema matarajio yake ni kufanya kazi bora zidi ya zile zilizopo nyuma huku akiwaomba mashabiki na wadau wa muziki wake kuendelea kuonyesha ushirikiano wa kuzipenda na kutoa ushauri kwenye kazi anazozifanya.

No comments