Habari

MTIBWA SUGAR YANASA SAINI YA BEKI WA ZAMANI WA SIMBA

on

MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mtibwa
Sugar wameendelea kujiimarisha dhidi ya msimu ujao baada ya kumsajili beki wa
zamani wa Simba SC Hassan Suleiman Isihaka.
Timu hiyo inayomilikiwa na kiwanda cha sukari bora nchini Mtibwa
Sugar kilichopo mkoani Morogoro, imefanikiwa kunasa saini ya beki huyo ambayo
msimu uliopita aliichezea kwa mkopo Afrika Lyon ya Dar es Salaam.
Hata hivyo baada ya Afrika Lyon kuteremka daraja msimu uliopita, Isiaka akafikia makubaliano maalum ya kuvunja mkataba na Simba ili awe huru
na hivyo kufanikiwa kujiunga na Mtibwa Sugar.
Ujio wa beki huyo ni pendekezo la benchi la ufundi la Mtibwa
Sugar linaloongozwa na Zuberi Katwila.
“Kiukweli usajili huu niliusubiria kwa hamu kubwa, nadhani
kila kocha anatamani kuwa na mchezaji huyu, nadhani bahati imedondokea kwa
Mtibwa Sugar pia natoa shukrani za dhati kwa viongozi kwa kufanikisha usajili
huu maana ulikuwa wa umuhimu sana kwangu,” amesema Katwila.
Kwa upande wake Isihaka amesema kwamba alikuwa anatamani kufanya
kazi na “Wana Tam Tam” Mtibwa Sugar kwa muda mrefu na anadhani amefanikiwa kwa kuwa ni klabu kubwa na wachezaji wengi nchini wakubwa
wamepita hapo.

Isihaka anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa na Mtibwa
dirisha hili wengine wakiwa ni kipa Shaban Hassan Kado, mabeki Salum Kanoni
kutoka Mwadui, Hussen Idd Hante kutoka JKT Oljoro, viungo Hassan Dilangu kutoka
JKT Ruvu na washambuliaji ni Riffat Khamis Msuya kutoka Ndanda FC na Salum.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *