MWANANDINGA MWINGINE KUTUA MAN UNITED KABLA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA

KOCHA Jose Mourinho amethibitisha kuwa anataka kuleta mchezaji mwingine Manchester United kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho alhamisi usiku.

United tayari wameshasajili wachezaji wapya watatu dirisha la majira ya joto Romelu Lukaku akitua kutokea Everton, Matic akitua kutoka Chelsea na Victor Lindelof akitokea Benfica. Zlatan Ibrahimovic pia amesaini mkataba mpya.

Lukaku ameleta mabadiliko ya haraka kwa mabao matatu katika mechi tatu za mwanzo Ligi Kuu Uingereza, wakati Nemanja Matic akiwa mwamba katika kiungo cha kati. Victor Lindelof bado hajacheza wakati Zlatan akitarajiwa kurejea dimbani mwakani.

Manchester United Evening News kilimnukuu Mourinho akisema kuwa hana mpango wa kuishawishi bodi kusaini mchezaji mwingine. Alisema:

"Kila mtu anatambua kwamba natamani kusajili mchezaji wa nne na siwezi kukataa hilo kwa sababu lipo kwenye akili yangu. Lakini bado nina furaha hata nisipopata mchezaji mwingine.

"Nilikuwa wa kwanza kuiambia bodi yangu kuwa hawana haja ya kupata presha kwa ajili yangu katika hilo.


"Labda msimu ujao, nitajaribu kusajili mchezaji katika sehemu ambayo nitaona inahitaji kuimarishwa."

No comments