MWANARIADHA USAIN BOLT AMWANIKA MRITHI WAKE MAPEMA... ni Wayde van Niekerk wa Afrika Kusini

BINGWA wa riadha duniani katika mbio fupi, Usain Bolt, amemtaja Wayde van Niekerk, kuwa mrithi wake kwenye mchezo huo mara baada ya kustaafu.

Bolt mwenye umri wa miaka 30, ametangaza kuwa baada ya kumalizika kwa michuano ya dunia ya riadha ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo hii mjini London, atasraafu mchezo huo.

Amedai kuwa mwanariadha ambaye anafanya vizuri na anakuja kwa kasi ni Niekerk raia wa nchini Afrika Kusini, hivyo anaamini anaweza kuja kuchukua nafasi yake ya ubora duniani.

“Van Nieker kwa kweli ameonyesha kuwa yeye ni nyota wa dunia, siwezi kumfananisha na mtu mwingine kwa kipindi hiki, ninaamini nikifanya maamuzi ya kustaafu yeye atakuwa ni mtu sahihi wa kuchukua nafasi yangu, sina wasiwasi na mwanariadha huyo,” alisema Bolt

Bolt amekuwa kivutio kikubwa cha riadha duniani baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mjini Beijing mwaka 2008.


Niekerk mwenye umri wa miaka 25, alishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kwenye mashindano ya olimpiki mwaka jana nchini Brazil huku akitumia sekunde 43.03.

No comments