MWIGIZAJI EMMA STONE AKIMBIZA MASTAA WENZIE WA KIKE KWA "MKWANJA" DUNIANI

MWIGIZAJI mahiri Emma Stone ndiye anayedaiwa kuwa staa wa kike ambaye analipwa  pesa nyingi zaidi miongoni mwa waigizaji duniani kwa mwaka huu.

Mwigizaji huyo aliyeigiza katika filamu iliyovuma sana mwaka huu ya La La Land alilipwa dola milioni 26 ambazo ni sawa na pauni milioni 20  katika kipindi cha miezi 12 kati ya Juni 2016 na Juni 2017.

Malipo hayo yalimfanya kuongoza katika orodha ya kila mwaka ya jarida la Forbes, na kuwashinda Jennifer Anniston na Emma Watson.

Jennifer Lawrence, aliyeongoza 2016, alikuwa wa tatu baada ya kulipwa dola milioni 24 sawa na pauni milioni 19.

Mapato ya Emma yalipanda kwa  asilimia 160 ukilinganisha na mwaka 2016, alipolipwa  dola milioni 10.

Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 28 majuzi alizungumzia mjadala kuhusu pengo la mishahara kati ya waigizaji wa kiume na wa kike, ambapo alifichua kwamba waigizaji wenzake wa kiume wameamua kwa hiari kupunguziwa mishahara ndipo walipwe kiasi sawa.


Jennifer Lawrence alikuwa ameongoza orodha hiyo ya Forbes kwa miaka miwili iliyotangulia, sana kutokana na ufanisi wa filamu za Hunger Games.

No comments