MWIGIZAJI EMMA STONE USIMPIMIE KWA MKWANJA DUNIANI

EMMA Stone ambaye ameigiza katika filamu ya ‘La La Landa’ anakadiriwa kuwa ndiye staa ghali zaidi wa kike Duniani.

Katika filamu hiyo peke yake alilipwa kiasi cha dola mil 20 ambayo ilitolewa kwa kipindi cha miezi 12, kati ya Juni 2016 na Julai 2017, kutokana na ufanisi wa filamu hiyo.

Malipo hayo yalimfanya kuongoza katika orodha ya kila mwaka ya jarida la Ferbes na kuwashinda Jennifer Anniston na Emma Watson.

Jennifer Lawrence aliyeongoza mwaka 2016, alikuwa wa tatu baada ya kulipwa dola mil 24.

Mapato ya Emma yalipanda kwa 160% ikilinganishwa na mwaka 2016, alipolipwa dola mil 10.


Jennifer Lawrence alikuwa ameongoza orodha hiyo ya Forbes kwa miaka miwili iliyopita, kutokana na ubora wa filamu za Hunger Games.

No comments