NADIA BUARI ACHEKELEA KUPIGA MZIGO NA RAMSEY NOAH

STAA mwenye mvuto kutoka nchini Ghana, Nadia Buari amesema kuwa amefarijika kufanya kazi na mwigizaji mkongwe kutoka Nigeria, Ramsey Noah.

Wawili hao wamekamilisha filamu ya “The Diary of Imesen Bown” ambayo imeongozwa na Jamel Buari.

“Imekuwa vyema kufanyika na Ramsey kwasababu ya uzoefu alionao kwenye sanaa, nadhani kila mmoja anatambua uwezo wake,” alisema staa huyo.


Katika filamu hiyo pia wamo mastaa wengine kama Zynell Zuh, Priscialla O. Agyemang, Jason El Agha, Henry Prempeh, Pasciline Edwards na d Lisbeth Lopez Acquah ambao wamecheza katika maeneo tofauti.

No comments