NAJ ARUKA KUMSHAURI BARAKA DA PRINCE KUJITOA ROCKSTAR 4000

MSANII wa Bongo Fleva na mpenzi wa Baraka da Price, Naj Dattani amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hakumshauri mumewe kuachana na lebo ya RockStar 4000 bali yalikuwa ni maamuzi yake.

Naj amesema Baraka sio mtu wa kushaurika kirahisi kwa mambo anayoamini yeye yana faida kwake, hivyo hata suala la kuachana na RockStar 4000 hakumshauri chochote.

“Sio kweli. Baraka sijawahi kumuingilia kwenye maamuzi yake na hata watu wanamjua kwamba sio mtu wa kushauriwa, yaani anakuwaga na maamuzi yake."

"Sometimes hata kuna vitu vingine mimi mwenyewe huwa ninampinga lakini yeye akiamua kitu, ameamua,” amesema Naj huku akisisitiza kuwa amemsapoti yeye kujitoa Rockstar 4000.

“Mimi ofcourse ninamsapport na ninamuamini anajua anachokifanya na asingetoka kama angeona kuna faida kwake, na yeye ni mtu ambaye yupo siriaz na kazi zake na anaamini kwenye kipaji chake so hataki kutegemea kitu ambacho hakimuingizii faida. Nilimuelewa na ninampa ‘support na maamuzi yake,” ameongeza Naj katika mahojiano yake na TBC International.


Hata hivyo Naj amewasibitishia mashabiki wa Baraka da Price kuwa kuna ngoma nyingi kali zinakuja hivyo wakae mkao wa kula.

No comments