NANDY APASUA KICHWA KUANDAA “MZIGO” UTAKAOFUNIKA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Faustina Charles “Nandy” amesema anaumiza kichwa kuandaa kazi mpya ambayo itakuwa bora zaidi ya "Wwasikudanganye".

Nandy amesema anajisikia vizuri kuona kazi zake zikizidi kukubalika kwa mashabiki, hali inayompa nafasi ya kujipanga upya kufanya nyimbo bora zaidi.

“Nimekuwa na mapokeo mazuri ya kazi zangu kwa mashabiki, hii inanipa moyo wa kuzidi kufanya vizuri zaidi." 

"Najua wimbo wangu wa “Wasikudanganye” umeendelea kufanya vyema,” amesema Nandy.


Nandy amekuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri hapa nyumani na kukubalika kwa mashabiki kutokana na aina ya nyimbo anazoimba.

No comments