NAU KALANDIMA QUEENS WATEMBEZA BAKULI

TIMU ya Netball ya Nau Kalandima Queen imeomba wafadhili kujitokeza kuipiga jeki ili kuweza kumudu gharama uendeshaji, ikiwa ni pamoja na vifaa vya mazoezi na mahitaji mengine.

Kiongozi wa timu hiyo, Fadhili Hussein Lugendo amesema kuwa kwa sasa timu inajiendesha kwa taabu kutokana na kushindwa kumudu gharama mbalimbali, hivyo anaomba wadau wa michezo kujitokeza kuwasaidia.

“Kama ambavyo inajulikana, uendeshaji timu ni suala linalohitaji uwezeshwaji mkubwa, nasi tumekuwa tukishindwa kupiga hatua kutokana na uwezo wetu kuwa mdogo,” amesema Lugendo.


“Tunaomba wadau wa michezo kutugeukia na kutusaidia ili tuweze kuyafikia malengo yetu kwani tumekusudia kufika mbali ila tunakwamishwa na suala la uwezeshwaji,” ameongeza kiongozi huyo.

No comments