NDOA YA NUH MZIWANDA YASAMBARATIKA IKIWA NA MWAKA MMOJA TU

NDOA ya Nuh Mziwanda na mkewe Nawal, iliyofungwa mwaka jana Novemba imeingiwa na kidudu mtu kilicholeta madhara na kupelekea ndoa hiyo kuvunjika.

Akizungumza katika U-Heard ya Clouds FM, wiki hii, Nawal amethibitisha kuachana na baba mtoto wake Anyagile na kila mtu anashi maisha yake na wakati huo huo amesema tayari yeye ameshaolewa na mwanaume mwingine.

“Sina mume mimi Nuh wakati anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukiristo) hakunishirikisha kwa chochote na mimi sasa hivi nipo kwa bibi yangu Msasani, pia nimeshaolewa na mtu mwingine,” amesema mrembo huyo.


Pia Nawal amedai kuwa mpaka sasa ameondoka alipokuwa anaishi na mumewe wake huyo, huku akidai mumewe ndio alikuwa na makosa katika ndoa hiyo pia tangia aondoke hapo akemkuwa hamjali motto wao kwa chochote kile pia Nawal ameelezea kuwa ana uwezo wa kumlea motto wake bila ya msaada wake kama aliweza kumzaa mwenyewe.

No comments