Habari

NEYMAR: NIMEJIUNGA NA PSG ILI KUPATA CHANGAMOTO MPYA

on

STRAIKA Mbrazil,
Neymar amesema kuwa alihitaji changamoto mpya  wakati anapojiunga na klabu ya PSG kutoka
Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha Euro miliooni 222.
 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda mataji
saba muhimu katika misimu yake minne katika uwanja wa Nou Camp ikiwemo taji la
klabu bingwa mara moja na lile la La Liga mara mbili.
‘Nimeshinda mataji yote niliohitajika kushinda” ,alisema Neymar
ambaye atapokea mshahara wa (pauni milioni 40.7 kwa mwaka katika kipindi cha
miaka mitano.
Akiandika katika mtandao wake wa Instagram, aliongezea:
Nimeshinda mataji yote ambayo mchezaji soka anafaa kupata.
”Nimeishi maisha ambayo siwezi kusahau, lakini mchezaji
anahitaji changamoto”.
”Na kwa mara ya pili katika maisha yangu, nitaenda kinyume na
matakwa ya babangu”.Uhamisho wa Neymar umevunja rekodi ya awali iliowekwa na
Paul Pogba aliporudi kuichezea Manchester United kutoka Juventus kwa kitita cha
pauni milioni 89m mnamo mwezi Agosti 2016.
Mshahara wake wa ni pauni milioni 782,000- kwa wiki unamaanishi
kuwa PSG itamlipa miliooni 400.

Neymar anatarajiwa kuzinduliwa mbele ya mashabiki wa PSG katika
uwanja wa Parc des Princes siku ya Jumamosi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *