NICHOLAS GYAN ASEMA ANA NDOTO KUBWA SIMBA SC

HUKUakifikiria kuomba uraia wa Tanzania ili aweze kucheza katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”, mshambuliaji mpya wa Simba Nicholas Gyan amesema ana ndoto kubwa katika Simba.

Gyan amekaririwa na vyombo vya habari vya nchini kwao Ghana akisema kwamba yuko tayari kuomba uraia wa Tanzania kusudi aweze kutumikia timu ya taifa ya Tanzania.

Lakini pia nyota huyo amesema kwamba anataka kuandika historia nyingine kubwa katika kikosi cha Simba kwa maana ya kuisaidia kutwaa ubingwa.

Pamoja na kutaka kuisaidia Simba kunyakua ubingwa, Gyan ambaye ni mdogo wake mwanasoka nyota wa Ghana, Asamoah Gyan amesema kwamba anataka kupambnana awezavvyo ili awe mfungaji bora wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara.

“Pamoja na kuisaidia Simba kuwa mabingwa, pia nataka kuwa mfungaji bora ili kuwaonyesha Waghana wote kuwa mimi kazi yangu ya kufunga naijua,” amesema.

Mshambuliaji huyo aliyetua Simba akitokea katika klabu ya Ebusua Dwarfs amesema kwamba amesiokitishwa kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana  “Black Stars” huku akiwa ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu.

Akihojiwa na waandishi wa habari nchini kwao Ghana, Gyan amesema kwamba ameshauliwa hata na ndugu zake kwamba kama kuna uwezekano aombe uraia wa Tanzania ili aweze kucheza timu ya Taifa baada ya kutoitwa kwenye kikosi cha ‘Black Stars’ B.

Kinda huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba na amefunga mabao 11 katika Ligi kuu inayoendelea nchini Ghana.

Tayari baadhi ya wachambuji wasoka hapa nchini wamemtabiria mshambuliaji huyo kuwa straika hatari zaidi hapa nchini kutokana na uwezo wake wakupambana na kufunga mabao.


“Akipewa nafasi ya kuonesha kazi yake Simba watakuwa wamepata bonge la straika ambaye atawasaidia sana katika mechi za kimataifa” amesema mmoja wawadau wa soka, Mosha Thomas.

No comments