NICK MINAJ, WIZKID WAZIDI KUJIACHIA KIVYAO

WAKATI sisi tunaona ni habari kumbe wao wala, msanii Wizkid raia wa Nigeria anazidi kukuza jina lake kimataifa hii ni baada ya kuonekana akiwa katika picha ya pamoja na mwanadada mkali wa Hip Hop duniani kwa sasa, Nick Minaj.

Wawili hao walionekana wakiwa wamekaa pamoja kwenye kochi huku Nicki Minaj akiwa kajiziba usoni na Wizkid aonekana akifurahia jambo, inadaiwa kuwa kazi inakuja baina yao.

Hii ni hatua kubwa kwa msanii huyo kutoka Nigeria kwani anaonekana kujitengenezea mianya mingi ya kuwashirikisha wasanii wakubwa wa Marekani katika kazi zake.


Wizkid tayari ameshafanya ngoma na wasanii wakubwa dunianikama Drake, Chris Brown na Trey Songz.

No comments