NIYONZIMA APANIA KUISAIDIA SIMBA KUBEBA UBINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU HUU


KIUNGO wa Kimataifa wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda amesema anataka kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anaisaidia timu yake kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. 

“Nimekuwa mwenye mafanikio katika timu zote nilizozichezea kuanzia APR mpaka Yanga na sasa niko Simba ambako nahitaji kufanya kitu kipya hapa kitakachoniweka juu,” alisema Niyonzima.

Niyonzima amesema kwamba anatambua ushindani wa Ligi ya Tanzania umebadilika na kuwa mkubwa tofauti na wakati ule niliojiunga na Yanga lakini hilo haliwezi kuwa kikwazo cha yeye kupata mafanikio akiwa na mabingwa hao wa Kombe la FA.

Kiungo huyo amebeba matumaini ya mashabiki na viongozi wa Simba wakiamini nahodha huyo wa Rwanda, atachangia kuwarudisha kwenye mafaniko yao ya zamani baada ya kufanya vibaya misimu minne mfululizo huku ubingwa ukienda Yanga mara tatu.

No comments