NIYONZIMA ASEMA MECHI NA MLANDEGE SI KIPIMO CHA UBORA WA SIMBA SC

KAMA unadhani kuwa matokeo ya Simba kutofungana na Mlandege kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar ndio kipimo halisi cha Simba, utakuwa umepoteza katika hesabu zako  za kufikiri tofauti.

Simba ilicheza na timu hiyo ya Unguja na kutofungana katikati ya wiki na baadhi ya mashabiki wa Simba wakawa na hofu kwamba ikiwa wanasuluhu na Mlandege itakuwaje katika Ligi kuu.

Lakini mmoja wa nyota wapya katika kikosi hicho, Haruna Niyonzima amesema kwamba hawana sababu ya kuangalia matokeo ya mechi hiyo, bali wao wanatazama mechi zinazokuja.

Akihojiwa baada ya mechi hiyo, Niyonzima amesema kwamba hawana wasiwasi na wala hawatazami nini kilitokea katika mechi hiyo bali wanaangalia mechi ambazo zinakuja mbele yao.

“Huo ndio mpira, umemalizika kwa matokeo hayo, lakini sisi hatuangalii haya tunatazama kinachokuja mbele yetu,” amesema fundi huyo wa mpira uwanjani.


Mnyarwanda huyo amesajiliwa na Simba akitokea katika timu hasimu ya Yanga, usajili ambao umewafanya mashabiki wa Yanga kukasirika na kufikia kiwanga cha kichoma moto jezi namba nane ambayo Haruna alikuwa akiivaa katika klabu yao.   

No comments