NJOMBE MJI WAJIPA UHAKIKA WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO LIGI KUU MSIMU UJAO

UONGOZI wa timu ya Njombe Mji umesema umoja na ushirikiano wa wachezaji katika kikosi hicho utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu watakazocheza nazo Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.    

Akizungumza jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Sofanus Mhagama alisema kipindi hiki cha mazoezi wachezaji wameonyesha kuelewana uwanjani na kuyafanyia kazi maelekezo ya walimu kwa kiwango kikubwa.

Alisema ushirikiano wa wachezaji umeongeza chachu kwa kocha wa timu hiyo kuendelea kutoa mbinu mbalimbali za kukifikisha mbali kikosi hicho.

"Wachezaji wanapojituma mwalimu anafarijika na kuona kuwa maelekezo yake yanafutiliwa kwa ukaribu, hicho ndicho kitu tunachojivunia."


"Kila mchezaji amepewa majukumu yake na anasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha anayatimiza, hivyo hatuna wasiwasi wowote tupo tayari kwa msimu ujao," alisema Mhagama. 

No comments