OFA YA EURO MIL 35 YA AS ROMA YADUNDA KWA MAHREZ... Leicester City wataka euro mil 45 kumwachia

TIMU ya AS Roma bado haijakata tamaa katika vita yake ya kumwania nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez, baada ya kutangaza tena ofa ya Euro milioni 35 kwa ajili ya kupata huduma ya straika huyo.


Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini England, bingwa hao wa zamani nao bado wameweka ngumu kuipokea huku wakishinikiza kuwa ni lazima zitolewe Euro milioni 45 ndipo watamwachia staa huyo.

No comments