OGOPA KOPA WAPELEKA UHONDO LINDI, MASASI NA NACHINGWEA


Kundi la Ogopa Kopa chini ya malkia Khadija Kopa, Ijumaa litakuwa Lindi mjini ambapo litaporomosha burudani katika ukumbi wa Bwalo la Polisi.

Ogopa Kopa ambao ziara yao imeanzia Alhamisi huko Kilwa katika ukumbi wa Kilwa Star, wataendelea na makamuzi yao siku ya Jumamosi Agosti 19 pande za Masasi ndani ya Rocky City Hotel.

Promota Dallas wa Masasi ambaye ndiye mratibu wa maonyesho hayo, ameiambia Saluti5 kuwa Ogopa Kopa watamalizia ziara yao Jumapili kwa show itakayopigwa Nachingwea katika ukumbi wa NR.

No comments