OWEN HAGREAVES AMTABIRIA MAKUBWA OSMANE DEMBELE

NYOTA wa zamani wa timu ya Bayern Munich, Owen Hagreaves amemtabiria makubwa straika mpya wa Barcelona, Ousmane Dembele, baada ya kusema kuwa ana uwezo wa kuwa kama Neymar na huenda akawa mshindi wa taji la mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or.

Akizungumza kuhusu Dembele, Hagreaves aliambia BBC kwamba staa huyo mwenye umri wa miaka 20 anaweza kuwa mchezaji bora kutokana na kwamba umri wake bado ni mdogo.

 “Amekuwa akisakwa lakini mtu yeyote ambaye amemuona akicheza nchini Ufaransa na katika ligi ya Bundesliga msimu uliopita atajua kwamba ni mchezaji mzuri sana,” alisema nyota huyo wa zamani wa Manchester United.


''Baki wengi watakuwa wakimuota. Kimaumbile ana nguvu na anaweza kucheza kwa kutumia miguu yote miwili.Anaweza kupiga mipira ya adhabu kwa kutumia miguu yote miwili'', aliongeza staa huyo wa zamani.

No comments