PAUL DYBALA SASA KUTINGA UZI WA ZINEDINE ZIDANE JUVENTUS

PAUL Dyabala amekubali kuikacha jezi yake namba 21 aliyokuwa akiivaa kwenye timu ya Juventus na kuchukua namba ya historia kwenye klabu hiyo ya Italia.

Dyabala atavaa jezi namba 10 ambayo iliwahi kuvaliwa na shujaa wa timu hiyo Alessandro Del Piero. Pia iliwahi kuvaliwa na kocha wa sasa wa Real Madrid, Zinedine Zidane pamoja na Roberto Baggio.

Mwanzoni mwa msimu uliopita mchezaji huyo kutoka Argentina alikataa kuvaa jezi hiyo huku akisisitiza ataendelea kuivaa namba 21 kama awali.


Mara ya mwisho jezi namba 10 ilivaliwa na Paul Pogba ambaye alijiunga na Manchester United baada ya kuivaa jezi hiyo kwa msimu mmoja tu. Mashabiki wa Juventus wanaonekana kufurahi, wanaamini Dyabala ni mchezaji sahihi kuvaa jezi hiyo baada ya Pogba kuondoka.

No comments