PEP GUARDIOLA NA HADITHI YA 'SIZITAKI MBICHI HIZI' KWA ALEXIS SANCHEZ


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amedai atakuwa na safu kali ya ushambuliaji hata kama atashindwa kumsajili Alexis Sanchez wa Arsenal.
Guardiola anamsaka kwa udi na uvumba Sanchez na tayari ameweka ahadi ya kumlipa mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki ambayo itakuwa rekodi mpya katika Premier League.
Lakini baada ya Arsenal kuonyesha kuwa imedhamiria kubaki na nyota wake, Guardiola anasema ana safu nzuri ya ushambuliaji chini ya Sergio Aguero na Gabriel Jesus.
Kocha huyo wa City anasema: "Nina washambuliaji wa kutosha, wanachotakiwa ni kutuliza tu akili na kufunga magoli.
"Nina washambuliaji wawili tishio, Gabriel (Jesus) na Sergio (Aguero), lakini ninao wengine pia ambao wanaweza kugunga magoli mengi".

No comments